THE ROCK AITAMANI IKULU YA MAREKANI

Muigizaji kutoka Marekani aliyekuwa mcheza mieleka maarufu duniani Dwayne Johnson ‘ The Rock ’ amezungumzia nia yake ya kutaka kuwa Rais wa Marekani kwakuwa anaamini anaweza.
Akifanya mahojiano na jarida la GQ ‘The Rock’ amesema kuwa amefikiria sana wazo hilo na kuelezea hali ya uongozi kwa upande wake kama jambo zuri ambalo linamvuti katika kuchukua majukumu ya watu wengi na kuwasaidia kimawazo hata kuwatoa hatua moja kwenda nyingine kwa maana ya kuwatengenezea maendeleo.
”Uongozi ni muhimu hasa pale unapokuwa na wadhifa wa kuchukua jukumu la kila mtu” Alisema The Rock.
Hata hivyo The Rock amaeungana na mastaa wengine wakubwa wakubwa duniani wenye nia kama hiyo ya kutamani kuhamia Ikulu ambao ni pamoja na Mkurugenzi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg, Jay Z na Kanye West.

Post a Comment

0 Comments