Ni idadi kubwa ya mashabiki wa muziki duniani ambao walidhani bado kuna hali ya kutoelewana kati ya marapa wa kike kutoka nchini Marekani Remy Ma na Nicki Minaj bifu ambalo liliwafikisha katika kuchanana katika ngoma tofauti zilizotoka hivi karibuni ambapo Remy amefunguka ya moyoni juu ya bifu lao.
Rapa huyo kutoka Brooklyn Remy kupitia msimu wa kipindi cha runinga cha
The Real amesema kuwa amemuondoa Nick Minaj katika orodha ya wasanii ambao anaweza kuwadiss. Remy pia amesema hana budi kusonga mbele na kuyaacha mambo yote ya kipindi cha nyuma yapite.
“Vumbi limetulia,” alisema. “Baadhi ya watu hawaelewi kwamba udongo umetulia. Ingawa siwezi kuelewa. Ni ngumu sana kuona vumbi limetulia unapokuwa katika kaburi chini ya uchafu. “
Aliongeza
“Yule ni Remy Ma wa zamani, nitakuwa mbaya zaidi kama nitaendelea. “Mimi nasema wakati wote, mimi ni mdogo. Lakini kuna mstari mwembamba unaotenganisha udogo na udhaifu hivyo inafika kipindi fulani mambo mengine unaacha.” Alimalizia Remy Ma kuhusu kumalizika kwa kutoelewana kwake na Nicki Minaj.
Hata hivyo mapema mwaka huu mambo yalionekana kuwa mabaya kwa wawili hao baada ya Remy kuachia wimbo uliokwenda kwa jina ‘Shether’ wimbo ambao ulimgusa Nicki Minaj ambapo naye hakukaa kimya akajibu na ngoma ‘Make love’ na ‘Swalla’ kisha Remy kujibu mashambulizi na ngoma ‘Another One’ picha mabalo halikuishia hapo kwani Nicki hakusita akaachia ‘No Frauds’ kolabo aliyowashirikisha Drake na Lil Wayne wimbo ambao inawezekana ukawa wa mwisho kuhusu bifu la wawili hao.
2
0 Comments