CHRIS BROWN NA TREY SONGZ WAMCHANA BOW WOW KWA KAULI HII

Bow Wow ameendelea kutengeneza vichwa vya habari Marekani na duniani kwa ujumla, bahati mbaya ni kwasababu mbaya. Awamu hii amedai kuwa ndiye aliyewatoa Trey Songz na Chris Brown. Wote wawili wamekanusha madai hayo.
Wakati akizungumzia issue yake ya kudanganya kwenye Instagran kuwa alisafiri na private jet, kwenye IG Live iliyonaswa na Baller Alert, rapper huyo alijigamba kwamba anastahili heshima kwasababu ndiye aliyewasaidia Trigga na Breezy kutoka kumuziki kutokana na kuwatambulisha kwa mashabiki wake miaka ya 2000s.
“They wouldn’t even know half these guys that they love today,” alisema rapper huyo ambaye jina lake ni Shad Moss. “I put Trey Songz on his first tour ever. I put Omarion on his first tour ever. I put Chris Brown on his first tour ever, which was The Scream Tour. Ciara, first tour ever was that.”
Bow anazungumzia ziara yake ya The Scream ya mwaka 2001. Kwenye ziara hiyo ilikuwa na misimu mitano ambapo Omarion, Chris Brown, Ciara, Jhene Aiko na Trey Songz wote walikuwa sehemu ya ziara hiyo iliyofanikiwa.
Baada ya madai hayo ya Bow, Trey Songz alitumia Instagram kujibu akiandika, “Ok, ok, I’ll do it. So Bow said what now?”
Naye Chris alicomment kwenye ukurasa wa Instagram wa Baller Alert, “somebody take bow phone.”
2

Post a Comment

0 Comments