Jux anataka watu waelewe kitu hiki ‘once and for all’, Trey Songz sio role model wake.
Amedai kuwa kitendo cha kujichora tattoo kifuani inayofanana na msanii huyo wa Marekani, hakimaanishi kuwa ni mtu anayemuangalia kwa jicho la ‘role model.’
“Trey ni mtu ambaye napenda tu kazi zake, sio role model wangu,” alisema muimbaji huyo wa Juu kwenye mahojiano na kipindi cha The Base cha ITV.
Kuhusu kilichotokea miezi kadhaa iliyopita kati ya Vanessa Mdee na Trey walipokutana Nairobi kwenye Coke Studio ambapo picha zao zilisababisha headlines nyingi, Jux anasema alikuwa anajua kila kinachoendelea.
“Niliona picha kabla hawajaona watu wote, kwahiyo nilikuwa najua kinachoendelea, kila kitu nilikuwa nakijua,” alisema.
“Mimi ni mtu ambaye naongea na Vanessa kuliko.. naweza kusema katika watu wanaongea mara nyingi na Vanessa mimi nipo, so updates nyingi sana huwa nazipata kabla ya watu wengine. Kwahiyo hakikunishtua kile kitu. Ila watu kuanza kuongea, natamani ningeweza kusema kitu fulani na kimfikie kila mtu na ajue kinachoendelea,” amesisitiza.
Hivi karibuni wawili hao wameachia video ya wimbo wao wa pamoja, Juu.
0 Comments