Aliyewahi kuwa meneja wa zamani wa Rich Mavoko, Papa Misifa amefuguka kwa kudai kuwa Rich Mavoko ni msanii ambaye hatakuja kumsahau mpaka anaingia karibuni kutokana na mambo aliyotendewa na msanii huyo.
Mkurugenzi huyo wa label ya Al Jazeera Entertainment ambayo inamsimamia, Killy, Aly Nipishe pamoja na Rhymes Biashara, amedai mpaka leo bado anamdai Rich Mavoko na kesi ipo Mahakamani.
“Mimi katika wasanii ambao sitawasahau katika maisha yangu ni Rich Mavoko, yule mtoto hana adabu,” Papa Misifa alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Mpaka kesho bado namdai na kesi ipo mahakamani. Yule tulipanga kwenda kushoot video Afrika Kusini, sasa kuna hela alikuwa nayo yeye akaondoka nayo,”
Pia Papa alidai muimbaji huyo hawezi kufanikiwa zaidi kwa kuwa tayari kuna mambo mabaya nyuma aliyafanya na anatakiwa kuyarekebisha pamoja na kuomba msamaha.
0 Comments