SHOLO MWAMBA AFUNGUKA CHANZO CHA UGOMVI NA MAN FONGI



Hakuna asiyefahamu kuwa kuna bifu zito baina ya wakali wawili wa muziki wa SingeliMan FongonaSholo Mwamba.Hitmaker wa ngoma ya GhettoSholo Mwambaametusanua chanzo na sababu kubwa iliyofanya wawili hao kuwa katika ugomvi huo mzito.Sholo Mwambaamedai kuwa sababu kubwa ya kutofautiana naMan Fongochanzo ni aliyekuwa bosi wao wote wawiliambaye niG Maker. Akidaiwa kuwa alikuwa na upendeleo na msanii mmoja ambaye niMan Fongobaada tu ya ngoma ya Hainaga Ushemeji kuhit, hivyo akaamini niMan Fongopekee ambaye anaweza kuwa na mafanikio makubwa.Sholo Mwambaamefunguka hayo kwenye kipindi cha Ng’ari Ng’ari cha Clouds TVhapo janaakihojiwa naSakina Lyokakwenye kipindi hicho.Sholoalidai kuwa yeye hana chuki kabisa na mwenziyeManFongoila tu ni tofauti za kibiashara ndio zinafanya asiwe na maelewano mazuri namshkaji wake huyo, na pia alidai kuwa hayuko tayari hata kidogo kumaliza bifu na Man Fongokwasababu ya kuupeleka muziki wa Singeli mbele kupitia bifu hilo.

Post a Comment

0 Comments