NEDY MUSIC SITAFANYA COLLABO NA WASAFI


Hit maker wa ngoma ya “Usiende mbali” na  mkali wa Bongo fleva kutoka lebo ya PKP Nedy music, ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngomayake mpya ya “Rudi” iliyotoka ndani ya mwezi huu akiwa na Christian Bella.Nedy MusicNedy Music, amesema hajafanya collabo yoyote na msanii kutoka lebo la Wasafi na wala hajafikiria kufanya hivyo.Nedy ametoa msimamo huo bila kueleza kwa kina sababu ya maamuzi hayo, alipokuwa katika kipindi cha FNL cha EATV baada ya kuenea kwa taarifa kuwa kuna collabo kati yake na msanii mmoja wapo kutoka Wasafi.Nedy ambaye ametoa ngoma yake ya pili chini ya PKP aliyoko pia Ommy Dimpoz, amesema taarifa hizo siyo za kweli na kwamba hana ugomvi wowote Wasafi, isipokuwa kinacho endelea ni masuala ya kazi tu.Kuhusu yeye kusalimiana na Wasafi amesema hana kinyongo na akikutana nao mahali popote atawasalimia“Nikikutana na Msafi (msanii kutoka Wasafi) yoyote nitamsalimia kama kawaida kama washkaji, lakini kama yeye hataonesha ushirikiano basi salamu itakuwa haina haja”

Post a Comment

0 Comments