NAY WA MITEGO AFAFANUA KUHUSU GHOROFA LAKE LA MILLION 300

Msanii wa muziki wa hip hop Nay wa Mitego amesema watu wanaoshangaa na kubisha gharama za ujenzi wa ghorofa yake kufikia zaidi ya tsh milioni 300 hawajui nini maana ya ujenzi.






Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Nay amedai yeye kwa kuwa anajua nini maana ya ujenzi hivyo hashangai kusikia mtu anajenga nyumba ambayo inagharizu zaidi ya milioni 300.
“Watu ambao wanashangaa nyumba kugharimu zaidi ya milioni 300 sijui niwaweke katika kundi gani,” alisema Nay. “Sema wewe huna pesa ya kufanya vitu kama hivyo lakini unavyokaa na watu ambao wanajenga nyumba za namna hiyo watakuwa wanakushangaa,”
“Mimi nyumba yangu ya Tabata ikikamilika gharama zote za ujenzi ni zaidi ya milioni hiyo 300. Tena kwa sasa ipo kwenye hatua nzuri, ni hatua ambayo inakula hela hatari kwa watu wa ujenzi wanajua nikiwa na zungumza hivyo ” aliongeza Nay.

Post a Comment

0 Comments