AFANDE SELE:DARASSA,ROMA,STAMINA,KALA WANAFAA KUVAA TAJI LA UFALME WA HIP HOP BONGO

Kwa mujibu wa Afande Sele, Darassa, Roma, Stamina na Kala Jeremiah, ni rappers anaoweza kuwakabidhi taji lake la Mfalme wa Rhymes.
Afande amedai kuwa kama shindano hilo likirudi tena, vijana hao wanaweza kuwa washindani sahihi kwa sasa.
“Naumizwa kuona kwamba Mfalme wa Rhymes ni tukio ambalo halifanyiki tena wakati watu wanataka lifanyike,” Afande alikiambia kipindi cha Ladha 3600 cha EFM. “Kwahiyo kipindi fulani tulikuwa na uhaba wa rappers wazuri lakini kipindi hiki kuna rappers wazuri kuanzia akina Darassa, Roma, Stamina, Kala wengi,” aliongeza.
“Kwahiyo Darassa, Roma, Stamina sizungumzii kufanya kazi, lakini naweza kuwapa hata ufalme wa rhymes.”


Mfalme wa Rhymes ni shindano lililofanyika mwaka 2004 na kuhusisha rappers mbalimbali wakiwemo Jay Moe, Profesa J, Inspector Haroun, Solo Thang, Madee, Mwana FA, Mandojo na Domokaya, Soggy Doggy na Dully Sykes aliyejitoea siku chache kabla ya shindano.
Afande Sele alishinda shindano hilo na kuzawadiwa gari.

Post a Comment

0 Comments