Picha: ALIKIBA ASHIRIKI KATIKA MECHI YA HISANI UGANDA ATUNUKIWA TUZO


Kama isingekuwa muziki, huenda Alikiba angekuwa mmoja wa vinara wa timu kubwa za soka nchini, zikiwemo Simba au Yanga.
Baada ya mechi, Alikiba alitunikiwa tuzo ya mchezaji bora staa
Pamoja na kufanya muziki, Alikiba hutumia muda wake mwingine kujikumbushia kipaji chake cha soka, na ndio maana Jumamosi hii alishiriki mechi ya hisani ya mchezo huo jijini Kampala, iliyopewa jina ‘A Celebrity For Charity.’ Mechi hiyo ilichezwa kwenye uwanja wa Kabira Country Club na kuhusisha nyota wengine akiwemo Emmanuel Okwi.
Timu ya Alikiba na Okwi ilishinda mabao 4-1 huku Kiba akifunga bao la 2.

        Alikiba akiwa na Jack Pemba na              promota maarufu wa Uganda
          Aly LAllibhai

“We won the game!!! White KingKiba team 4 The Green Team 1
Second goal courtesy of your King. Thank you Uganda for the Award for Best Celebrity Player Award,” ameandika Alikiba kwenye Instagram

Alikiba akiwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi

Post a Comment

0 Comments