Ni ukweli kuwa muziki wa Hip Hop nchini kwa sasa umeanza kurudisha makali yake baada ya baadhi ya wasanii kuonekana kubadilika kwa kuachia kazi zinazogusa watu wote. Rapper Nay wa Mitego amemsifia Songa na kumfananisha na Darassa.
Rapper huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa ameupenda wimbo mpya wa Songa ‘Mwendo Tu’ ameonekana kwenda alipofika hitmaker wa Muziki, Darassa.
“Nimesikiliza na kuiona ngoma mpya ya Songa kiukweli nimeiipenda naona Songa anakwenda alipo Darassa sasa safi sana. Tufanye muziki wa pesa kama hivi mambo ya misingi sijui tuiweke pembeni,” amesema Nay.
0 Comments