Kwenye interview niliyofanya na Joh Makini wiki iliyopita nilimuuliza iwapo safari yake ya Afrika Kusini hivi karibuni ilikuwa ni kwaajili ya kushoot video ya wimbo aliomshirikisha staa wa Nigeria, Davido lakini hakuwa tayari kusema.
Na sasa huenda Nahreel, producer wa wimbo huo anaweza kuwa na jibu la status ya wimbo huo ulioanza kuzungumziwa kitambo.
“Hii ngoma inaenda kutoka na Joh Makini nadhani ameshashoot video manaake alienda South Africa juzi juzi hapa wameshashoot kwahiyo stay tuned inakwenda kutoka,” Nahreel aliambia E-News ya EATV.
0 Comments