Q, CHIEF KUWEKA KAMBI SA KUSHOOT VIDEO YA KOKU FT PATORANKING

Msanii wa muziki Q Chief amedai wiki ijayo anatarajia kusafiri kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kushoot video ya wimbo wake ‘Koku’ aliyomshikisha msanii wa Nigeria Patoranking

Muimbaji huyo ambye yupo chini ya label ya Qs Mhonda Entertainment, ameiambia Bongo5 kuwa analazimika kufanya video ya wimbo huo kutokana na mashabiki wa muziki wake kuipenda kolabo hiyo.
“Mungu akipenda tarehe 17 mwezi huu nitasafiri na uongozi wangu kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kushoot video ya wimbo Koku niliyomshirikisha Patoranking, ni wimbo ambao umependwa sana na mashabiki, sasa ningependa uishie kwenye audio bila video,” alisema Q Chief.
Disemba mwaka 2016 muimbaji huyo aliachia video ya wimbo wake ‘Sungura’ ambayo bado inaendelea kufanya vizuri.

Post a Comment

0 Comments