Kituo pendwa cha Runinga nchini Nigeria cha Soundcity kimeandaa tuzo zake zijulikanazo kwa jina la Soundcity MVP Awards na kwa mwaka huu tayari orodha ya wasanii watakao tumbuiza kwenye sherehe za ugawaji wa Tuzo hizo majina yameshatajwa.
Kwenye orodha ya majina hayo mpaka sasa hakuna msanii hata mmoja kutoka Tanzania ingawaje bado list ya wasanii watakao tumbuiza inaendelea kutajwa.
Majina hayo ya wasanii waliotajwa ni pamoja na Davido, Patoranking ,
Olamide , Nasty C na Tekno ambao wote wanatoka Nigeria isipokuwa Nasty C tu ambae anatoka Afrika Kusini.
Tuzo hizo ambazo zitafanyika Tar 29 Desemba 2016 Jijini Lagos nchini Nigeria, Tanzania tutawakilishwa na wasanii wanne tu ambao ni Diamond Platnumz, Vanessa Mdee , Alikiba na kundi la Navy Kenzo .
Zoezi la upigaji ni mpaka December 27
0 Comments